Category Archives: Hardnews yaliojili

DAMU YAKO DAUDI MWANGOZI HAITAMWAGIKA BURE

UTPC Yaanzisha tuzo ya Mwangosi

Sasa nimeona walau ule usemi ulioandikwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (IPC) sasa waonekana utawafuta machozi waliokuwa wanalia waliopoteza, waliokatabtamaa. Hii ni chachu, Daudi anaishi milele. Kweli hii ni namba yako

Na Rogers Willium,

Mwanza

Umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania UTPC umeanzisha tuzo ya ushujaa na utumishi uliotukuka ya mwandishi wa habari marehemu Daudi Mwangosi aliyeuawa mwaka jana.

 

Tuzo hiyo inaanzishwa kufuatia kuwa mwandishi wa habari kwa kwanza Tanzania kuuawa akiwa kazini katika vurugu za polisi na wafuasi wanaodaiwa kuwa ni wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo mkoani Iringa.

 

Tuzo hiyo ambayo itakuwa ikitolewa septemba mbili kila mwaka itamfanya mshindi kuibuka na shilingi milioni 10 pamoja na cheti.

 

Tukio la kutangazwa kwa tuzo hiyo ya Daudi Mwangosi ilifanyika jijini mwanza ambapo bodi ya Umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania ndio ilipitia mchakato mzima wa kuanzisha tuzo hiyo huku ikiwa na vigezo zaidi ya vinne ili kuweza kufanikiwa.

 

Waandishi wa habari wa Magazeti, Radio, Television, Vijarida na Blogi ndio watakuwa na wasaa wa kuwania tuzo hizo huku bodi ya UTPC ikiwa ndio yenye jukumu la kumtafuta mtu atakayeweza kuibuka kinara.

 

Kuuawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi aliyekuwa akikitumikia kituo cha Television cha  Channel ten mkoani Iringa kunaufanya Umoja wa vyama vya waandishi wa habari kuwa na mtazamo wa kuweza kuwalinda wanahabari katika matukio yanayohusisha vurugu na maandamano.

 

Tuzo ya ushujaa na utumishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi inatajwa kuwa kifuta jasho kwa waandishi wa habari,hasa wakiitupia macho sheria ya uhuru wa vyombo vya habari kama kikwazo.

 

Kifo cha Mwandishi wa habari Daudi Mwangosi kilitokea septemba 2 mwaka jana na kuleta simanzi katika tasnia ya habari na nchi kwa ujumla.

Advertisements

Bodi ya mikopo na matatizo ya wasomi wa UDOM

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Udom wamekuwa ktk wakati mgumu san baada ya Boad kutotoa pesa ma mafunzo kwa vitendo. Wanafunzi hao walikutana shule ya Sekondari Meta leo tarehe 14/07/2010 wakiimba wimbo maarufu wa maombolezo ya Baba waTaifa. Kama sio juhudi zako Nyerere…. kamasio juhudizako nyerere….

Sisi tunahoji azma ya bodi ya mikopo ni kujenga mazingira mazuri ya kujifunza au ndo kikwazo? Tunaona migogoro na migomo imeongezeka hadi katika taasisi binafsi tangu kuanza kwa tasisi hii ya mikopo.

Pia hivi hawa UDOM si ndo wale walio mchangia Rais fedha za formu ya urais ndani ya CCM? Je sio hawa walioona JK ndio suluhisho la matatizo yote kimsingi JK amefanya kilakitu zaidi ya matakwa yao……. iweje leo wanalia wakimkumbuka Mwalimu Nyerere???? Hapa wanatuchanganya sana haytuelewi wanachosimamia wasomi hawa.

Au bodi walipoona hawa wasomi baada ya kutumia bumu kwaajili ya masomo wakaamua kupigia politic Boadi imetaka kuwafundisha somo???? Ohh no  Rais ndo ameweka Bodi sasa bajeti ya bodi imeenda wapi mpaka manteletual hao walie njaa? Wamepanga kwenda kumwona Mwakipesile Mkuu wa Mkoa kumwomba nauli.

Je suluhisho la matatizo haya ndo kuwa na benk za biashara zinazotoa mikopo kwa wanafunzi nchini?? Benku ya nani? Kwaajili ya nani? Riba kwa manufaa ya nani?

KAMPENI ZA KISTAARABU??????

Mzee wa vipaumbele. Mgombea Urais kwa tiket ya CCM Zanzibar Mheshimiwa makamu wa rais Dr. Ally Mohamed Shein, ametoa kipaumbele chake cha kwanza kuwa kampeni zake zitakuwa za kistaaraabu!!!

Sie kutahamaki na kung`aka alas kumbe miaka mingi hakukuwa na kampeni sa kistaarabu?? Nani hakuwa na kampeni za kistaarabu? Bila shaka zitakuwa za CCM ndo maaana ameanza mapema kuwaambia wenzake ili ashinde hatatumia kampeni za kishenzi (Kinyume cha ustaarabu). Kama sio CCM ni nani? Wapinzani?? Kama wapinzani Selikali ya CCM ilikuwa wapi? Selikali imekuwa ikiweka uwanja “sawa” wa ushindani!!! Kama ndivyo yanini kuwaweka hawa jamaa wasio weza kuweka ustaarabu ktk uchaguzi? Kwakuwa CCM imeongoza tangu huko miaka ya sabini, na kama hi indo stail yao mhhh how can you teach the old dog new techniques??? Sie tuna hoji tu nyie mwaweza tusaidia sie tuna mashaka katika hili ndio maana tunauliza tu ilitufahamu .

SASA NI RASMI SERIKALI YABWAGA MANYANGA KUSOMESHA

Waziri wa elimu mh Prof. Maghembe ametangaza bungeni kuwa selikali ipo katika hatua za mwisho za kuhakikisha mikopo ya elimu ya juu hutolewa na Benki za biashara nchini. Hii imekuwa dhairi sasa wakati wanafunzi na jumuiya ya chuo kikuu cha dar es salaam mwaka 2004 wanagoma kupitisha muswada wa kuanzisha bodi ya mikopo walidai serikali inajitoa kusomesha wananchi wake wakati ingeweza somesha wote bure kabisa bila mikopo. Selikali ilipinga hilo sasa miaka sita tu hali ipo wazi kazi kwenu wananchi.

Hapa tuauliza tu mikopo kutolewa na benki za biashara sisi tuliotoka ktk Kanumba Academy na familia za kafie mbewle tutafika Vyuoni??? Nadhani elimu ya juu itakuwa anasa kwa walio wengi muda simuda.

Swi mnafahamu wangapi wameacha masomo kwa hili la mikopo kwa muda huu??? Si mwajua  kuna wengi wamepewa mikopo wakati hawastahili wakati wahitaji wameachwa nje??

HAYO YALIFANYWA NA  taasisi isiyo hitaji faida ni ya selikali, itakuwaje kwa taasisi ya biashara?? Yale masuala ya dhamana na riba yaliyo ktk sheria ile sasa nadhani ndo mahali pake. Mie nauliza tu mwaweza jibu napengine toa taarifa tofauti.

Wakusoma nae Atangaza nia

Mwenye shati ya kijani Pichani ndiye aliye jitangaza nia ya kuwania ubunge CCM Ludewa- picha akiwa maelezo- Majira

Habari zilizojili kupitia vyombo vya habari nikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo kikuu cha Dar es Salaaam sehemu ya mlimani Zakayo Mepuyinywe ametangaza nia ya kugombea ubunge ktk jimbo la ludewa katika mkoa mpya wa Njoluma kando ya Ziwa Nyasa.

Ikumbukwe kuwa Mbunge wa sasa wa jimbo hilo ni Profesa Rafael Mwalyosi ambaye pia alikuwa Prosefa wa chuo hichohicho na hatatangaza kutoendelea.

hapo sasa mwalimu na mwanafunzi wake waenda kuchuana. kazi kwao wapigakura wakiamua kumchukua mwalimu au mwanafunzi. lakini kuna Deogratius Haule filikunjombe pia nae ametangaza nia ya kumg`oa Profesa.

Swali la kujiuliza kunanini Ludewa??????? watuhawa wote watatu na wengine wengi wenye nia au ambao watatangaza nia wanania ya dhati kutumikia wananchi??? Au kuna biashara huko??? sie tunahoji tu wajibu wakupima ni wa wanaludewa wenyewe.

Profesa mwalosi anawaonaje hawa wanaoitwa mavuvuzela wanaoongezeka????? mie mhhhh kazi kwenu nadhani Mtikila atatangaza nia tu sijui. anyway kazi kwenu CHAGUENI KILICHO BORA KWENU SIO KWA CHAMA.

Uchaguzi wa wagombea wa CCM

tangu tarehe 10 kumekuwa na heka heka wengine wanaita CCM congress, wengine wanaita CCM concert. Mkutano au tamasha full of mipasho na vijembe ndani ya chama chama chenyewe na nje ya chama.

enewei, mwisho tumepata yale tuliyo taraji kuwa kuwa na wagombea uongozi wa nchi kupitia CCM.

Juma mosi tarehe 10/7/2010 walituleteoa Dr.Ally Mohamed Shein kama mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama hicho kwa Zanzibar

Jumapili ya tarehe 11/7/2010 wametuletea Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mgombea Urais Wa Muungano kwa awamu ya pili.

siku hiyohiyo walitutangazia Dr. Gharib Bilali kuwa mgombea mwenza.

sie wenye mashaka tunahoji hayo ndio maamuzi wa watu walioamua kwa hiari yao bila shuruti kwa maslahi ya taifa wakidhani hawa ni wawakilishi wao ambao watalinda maslahi ya taifa. hoja ngumu lakini wengine wanauliza maslahi ya taifa ninini??

huu ni mwanzo karibuni tuhoji zaidi

KARIBUNI

safu ya milima ya livingstone

Karibuni katika jukwaa hili!!!!!!

Hapa kazi yetu ni kuuliza tu. Tunauliza kilakitu chenye maslahi kwa jamii yetu. Tunahoji hata kuhoji kwenyewe kwakuwa tumepata tetesi za hoja nyingine zinakuwa na mashaka hoja zenyewe nazo huhitaji hoja kupata hizo basi tumeona vyema tuhoji hata hoja zenyewe na mchakato mzima wa kuhoji ilikupata maendeleo yetu wenyewe.

Karibuni sana

Evaristo, H.E. E