Tathmini ya mbinu zakijamii za kukabiliana na maafa ya kijiolojia katika maeneo ya jirani na Oldoinyo Lengai, kaskazini mwa Tanzania

Na Evaristo H

IKISIRI ya tasnifu

utafiti huu umenuia katika kutathmini mbinu za kijamii za kukabiliana na maafa ya yatokanayo na miamba katika maeneo ya jirani na Oldoinyo Lengai, kaskazini mwa Tanzania. Utafiti huu umetumia kiunzi cha nadharia ya haki ya kutumia rasilimali na kuelezea chanzo cha maafa kwa ujumla wake. Utafiti  huu ulitumia data fuatilizi kutoka katika makavazi za jiolojia, picha za satelaiti na maktaba mbalimbali. Umetumia pia data za msingi kwa kupitia majadiliano ya makundi, mahojiano ya kina na dodoso ili kupata uhalisia toka kwa wahusika.

Utafiti umebaini kuwa jamii inauelewa wakutosha juu ya hatari ya maafa na kuweza kuya chambua maafa katika makundi kadhaa.  Ilifahamika kuwa maafa husababishwa na mwenendo mbaya wa maisha ya mwanadamu dhidi ya binadamu mwenzake na Mungu (Lengai). Kuna milipuko ya volcano ya kawaida ambayo haileti maafa. Milipuko hii hurutubisha ardhi  na huua wadudu wanaoathiri mifugo. Aidha kuna milipuko na matetemeko ambayo huathiri watu na mali. Athari hizo nipamoja na vifo vya watu na wanyama, kujeruhiwa kwa watu na wanyama, kuhabiriwa kwa makazi, malisho, barabara, vyanzo vya maji, shule na zahanati. Uchafuzi wa hewa kwa vumbi na hewa ukaa na kuhama kwa watu ni baadhi ya athari hizo.

Watu wamejifunza maumbile ya ikolojia ya Oldoinyo Lengai na kuweza kubashiri kinachoweza tokea kwao. Elimu hiyo hutambulika kupitia masimulizi ya miaka mingi yaliorithishwa toka kizazi hadi kizazi na kupitia Olaiboni watu wenye nguvu ya kuwasiliana na Mungu na kung`amua alama za maumbile hayo.

Pamoja na yote hayo jamii bado haina uwezo wa kutosha wa kukabiliana na maafa kwakuwa  haki yao ya kumiliki na kutumia mali yao kidemokrasia imebinywa. Hawana uhuru juu ya rasilimali zilizopo na kusafiri hasa maeneo ya hifadhi, hawana haki ya kutumia ardhi kadiri ilivyo pasika. Hakuna mfumo wa kisasa wa kuthathmini maafa na kutoa taadhari. Serikali hainabudi kuelewa mbinu za wananchi na kuangalia namna bora ya kuboresha kwa pamoja. Samabamba na hilo taasisi mtambuka za kuweza kusimamia mbinu mijarabu za kuzuia, kupunguza na kujiandaa na maafa ziweke katika jamii husika.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: