ALIESHIKWA NA KAMBA, KWANI NDIE MLANYAMA?

ALIYESHIKWA NA KAMBA

Na Evaristo Haulle

Kisima cha mashairi, ulilosema yakini

Kuchinja usikariri, yachunguze kwa makini

Tulikuwa na buheri, kwa miaka machinjoni

Nimekushika na kamba, kwani wewe mlanyama?

 

Kabla huja mega tonge, kwa kitoweo cha mbuzi

Akili yako ikonge, muwaze mfuga mbuzi

Tafika mchafukoge, usipofanya ajizi

Nimekushika na kamba, kwani wewe mlanyama?

 

Kama mwashirikiana, wakristo waisilamu

Sasa mbona mwagombana, inatoka wapi sumu

Kama kweli mwamegana, au imeisha hamu

Nimekushika na kamba, kwani wewe mlanyama?

 

Tafuta yaliyochanzo, usije kamwacha mwizi

Kautatue mzozo, alo na kamba si mwizi

Kamba ni dogo tatizo,  mtafute mwizi mbuzi

Nimekushika na kamba, kwani wewe mlanyama?

 

Fukua chini ya jivu, moshi kamwe si dhahili

Na uondoe uvivu, mapigano hayanadili

Utaupata welevu, moto ukiwa dhahili

Nimekushika na kamba, kwani wewe mlanyama?

 

Mchawi mtafuteni, maji yaje mikononi

Tuirejeshe amani, kabla mkono kinywani

Ufikapo hotelini, wewe tu peleka pwani

Nimekushika na kamba, kwani wewe mlanyama?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: