Monthly Archives: March, 2011

DAWA YA UKIMWI IMEPATIKANA??/

tANGU MWEZI aUGUST 2010 KWA NAMNA ISIYO YA KAWAIDA TENA BILA MBWEMBWE WATU WAMEKUWA WAKIFURIKA HUKO Loliondo kwaajili ya kupata dawa ya magonjwa sugu ikijumuisha dawa ya ukimwi ambayo hupatikana katika mchanyato wa kimiminika kinachotokana na kuchemsha mitishamba na maombi ya ibada. Mchanyato huu wa ainayake umeleta hamasa yaajabu mwezi februari mwishoni na march mwanzoni.

mchanyato umeleta tafrani kufanya watu wawatoe wagonjwa wao ktk hospitali na kuwapeleka kijijini Samunge kwa Ambilikile Masapila.Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT),

nauli zimepanda balaa, maisha hayakamatiki tena huko, ofisi hazikaliki tena mjini wote wanataka kwenda kupata KIKOMBE cha mchanyato huo.

waliotoka huko na wale wenye ndugu wa jirani tumewasikia wakisema wagonjwa wao wamepata nafuu kutokana na dawa hiyo na wengine kupona kabisa ingawaje nieleze sijapata ushuhuda bado wa mtu aliyekuwa na ukimwi akatangazwa amepona kadhalika wale waliokuwa wakisumbuliwa na saratani.

 

Hoja yangu hapa si kuangalia nini hasa kinatokea huko ila hilo nikwali ntakalo jiuliza baadae sana. swali nililokuwa najiuliza kila mara kabla ya tukio hili naona ni muafaka leo hapa.

 

Je kama kweli dawa hii yatibu na au dawa madhubuti ikipatikana jamii itakuwaje?? watu watakuja na tabia gani juu ya maisha yao??

nasema hivyo kutokana na ukweli kuwa maadali yamepungua sana siku hizi. watu hufanya matendo ya ngono hovyo bila hofu ya ukimwi nahoji itakuwaje kama ukimwi utapata dawa??? itakuwaje kwa wale wanaohofu si kwasababu sio maadali bali ni kwasababu ya ukimwi itakuwaje hapo? mie nauliza majibu sina hata sijapata fikiri kwakuwa sikuweza fikiri sana juu ya maisha ya jamii kabla ya ukimwi na hali ya maadili ya kitaifa kwa kipindi hicho

´╗┐

chungaji mwenye kikombe akiwa na msaidizi wake

Advertisements