Monthly Archives: September, 2010

JK DHARAU na UTANI HADI LINI?

JK  ameahidi kununua bajaji 400 ilizitumike kama magari ya wagonjwa. Ameahidi kupunguza tatizo la akina mama wanaokufa kutokana na uzazi. Si waungwana mwajua kuwa takribani wanawake 69 kila 1000 hufa wakati wa kujifungua? si mwajua MKUKUTA uliahidi kupunguza vifo hivyo kufikia 58 kwa juni 2010? manake ilani ya muheshimiwa ilichemka. si mwajua ilani na MKUKUTAvyote ni vya miaka mitano?  Manake JK hajafanya la kupasika sivyo???/ Inakuwaje twafikiria Bajaji. hebu waungwana fikirieni juu ya Bajaji za kubeba wagonjwa. Sijui mie mbumbumbu wa teknohama. mie sijui vyema teknolojia. sijui bajaji zipi anazozizungumzia Rais huyu anaye maliza muda wake? hizi tunazi zijua? Hizi zilizo finyu hata mtu mzima lazima ajikunje? bajaji zipi? hata hizi zinazoongoza kwaajali mijini??? nadhani anataka kuongeza idadi ya wanao kufa kwa kujifungua kwaajali. labda muniambie Ni bajaji za namna yake. hizi Bajaji kwa njia zipi? mie nauliza tu nielekezwe amesema atanunua gari moja tu la wagonjwa miaka mitano?????? mhhhhh!!!!!

Advertisements

POLENI CHADEMA

Nimekuwa nafuatilia kwa makini kidogo mambo yanavyoenda ktk uchaguzi huu.

nimegundua hali ya CHADEMA NIMBAYA SANA KULIKO VYAMA VINGINE VYA UPINZANI

Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana. ni nini wagombea wa CHADEWA hunadi kwa wananchi? mara nyingi nikisikiliza hasa kupitia kituo chetu cha taifa maranyingi hatusikii alichoongea mfano juzi walikuwa wanamuelezaa juu ya helikopta ya Dr. slaa kupata mushkeli lakini hawakusema lolote lililotokea katika safari yake. mpaka nashawishika kutaka kusomea uandishi wa habari. nahisi wanashindwa kutafuta stori ni nini katika safari nzima na tatizo la ndege kuwa kijazio tu. tofauti na Prof. Lipumba walijitahidi kumripoti vyema huko mtwara akieleza vizuri juu ya maendeleo ya kilimo. achilia mbali namna wanavyo mkava JK ni zaidi ya kufuru. simnajua ilekitu iliyoandikwa juu ya waandishi wa TZ kulamba miguu ya JK.

Sasa ni suala la elimu wajua sasa wamekuwa bize kumkabidhi JK  udaktari wa falsafa PhD labda afananie na udaktari wa Slaa. Slaa jamani ni mwana zuoni msomi sio sawa na shahada za heshima?!!!!!! wenye shahada za heshima hawaitwi kwa jina hilo jamani!!!! TCU mpo wapi hapo????

Jambo la ndoa na uzinzi wa Slaa. nani leo anazungumzia iletabia ya totoizi ambayo ilifungamana na JK kwa kipindi cha nyuma?? Je mnataka kutusadikisha ameacha?? Nani anazungumzia uzunzi huu???? stori za wake zawatu nimpya hapa?? au Afrika ya kusini???

Mie nauliza kitu kimoja kikubwa wanasheria nisaidieni Ndoa ni nini? Je sio ni mkataba? Je sio mkataba kati ya mume na mke? nani anayehusika kufrastrate mkataba kama sio wasaini wa mkataba? Je Slaa kama mgombea uraisi moja kwa moja anahusika? amebaka??? mpaka ashitakiwe?? Slaa anashitakiwa kwa sababu ipi wakati yeye sio miongoni mwa pande za mkataba huo. nadhani alitakiwa kumshitaki Josephine sio Slaa labda. Lakini inakuwaje kulazimisha penzi?? Je Josephine sio binadamu mwenye utashi ambaye anajua anachofanya? Nadhani hapa huyu anaeitwa Bwana  wa Josephine na wapambe wake wamemwona mwanamke ni bidhaa inayoweza gombaniwa na sio kama binadamu anayeweza fanya maamuzi. kama ndivyo hivyo hata katika shitaka anatakiwa kushitaki mtu ambaye alimsaidia yeye kupata hicho kifaa kiitwacho josephine. sijui wale wanaharakati wa haki za Binadamu na Wanawake wanasemane katika hili mie nauliza tu waungwana tusaidieni kuuliza ilitupate muafaka

Nashawishika kuwa ni hujuma tu na kwamantiki hii nachelea kuita uchaguzi ujao ni wahaki wakidhani CUF sio tishio kubwa na CHADEMA ndo tishio. Pili kwakuwa ndoa na CUF imefingwa Zanzibar inaweza tumika hadi Bara kimtindo mie sijui nauliza tu.

SOKO LA KARIAKOO NI MALI YA NANI?

Waungwana mie nauliuza lile soko la kariakoo ni mali ya nani? Nahoji hivyo kutokana na sababu kuwa nafahamu kuwa Si ruksa kwa majengo na ofisi za selikali hazistahiri kubandikwa mabango ya wagombea uchaguzi. kwa siku nyingi nilijua Soko la karia koo ni mali ya umma. Kama ni shirika la umma inakuwaje picha za JK mgombea uchaguzi kwa tiketi ya CCM yabandikwe ktk jengo hilo. lakini cha kuhofu zaidi mabango hayo yamebandikwa ndani na sio nje ya jengo hilo. je kubandika ndani ya jengo hilo sio mbinu ya kujificha?? kwanini yabandikwe humo katika jengo la umma? nisaidieni waungwana kunifahamisha taratibu na ukweli juu ya soko la Kariakoo. mie nauliza tu