Monthly Archives: August, 2010

WAZIRI MASHA AJIUZULU

Sisi tumeangalia mchakato wa uchaguzi jimboni ilemela tumeangalia na kuhoji na kuwa na mashaka na uhalali wake. TUMEBAINI HANA SABABU YA KUTUONGOZA KWAKUWA SIO MWAMINIFU

Pamoja na kuwa na tuhuma ya kumtisha mgombea wa CHADEMA jimboni hapo ajitoe, pamoja na suala la kumtisha aache kazi bado alifanya jambokuubwa zaidi la ajabu ambalo mgombea huyo hakupasika kulifanya.

Ukizingatia kuwa Masha ni waziri wa mambo ya ndani anahusika na ulinzi na usalama wa raia. Anahusika na masuala ya uhamiaji.

Mgombea huyu amekuwa kwa muda mrefu kama waziri na Mbunge kama alivyo sema mwenyewe alikuwa anaongea na Mgombea wa CHADEMA kama mdogo wake akimshauri ajitoe. Hii inamaanisha alikuwa anamfahamu fika. Tunachohoji hapa nikwamba kwanini leo Masha ampelekee pingamizi la ulaia wa mtu huyu ambaye amemfahamu kwa muda mrefu tu????

Tunauliza hapa kwani huyu mgombea maeanza kutokuwa mtanzania  lini? Je ameacha kuwa mtanzania pale alipo gombea?

Kama kweli tangu muda mrefu mgombea huyu sio mtanzania basi Masha ajiuzulu kwakuwa hakufanya kazi inavyopasika aliwezaje kuishi na watu waliojiita watanzania wakati sio watanzania. Watanzania hatuhitaji waziri kama huyo, waziri asiyewajibika asiyejua unyeti wa wizara yake. Ni waziri asiye faa hakuwashauri vizuri CCM kama mtu muhimu sana juu ya uraia wa Bashi.

Kwakuwa Masha bado ni waziri tunataka waziri huyo ajiudhuru maramoja.

Advertisements

HARAKATI ZA KUSHIKA HATAMU ZAANZA

Huku JK Mgombea wa CCM akianza kampeni zake kama alivyo kuwa akifunga kampeni zake mwaka 2005 kwa kuanguka Hawa nao wanaanza kampeni yao kwa kutonesha majeraha na kuomba apigiwe kura Slaa

Yes We Can Bring the Change We Need by Voting to the Right Candidate.

Nikikumbuka matusi niliyotukanwa kama mfanyakazi kwa kudai haki yangu,tena jasho
langu yaani KODI yangu.
Na mengine mengiii…….Kama wewe ni mfanyakazi au miongoni mwa wanaomtegemea
mfanyakazi kwa namna moja au nyingine,huna budi kumpigia kura Dr.W.Slaa,
Jakaya ameshasema yeye HAITAJI kura za wafanyakazi.Na hata mkigoma kwa miaka
nane hiyo mishahara hamtapata.Lakini yeye yupo tayari kutumia BILIONI 25 kwa
safari za nje tu!!!!! achilia mbali za ndani na sherehe zisizo na kichwa wala
miguu.
Ndugu WATANZANIA wenzangu ni wakati wa kuamka sasa kupambana na MAFISADI na wala
kodi zetu bila ya hata kuvuja jasho kwa kuongea maneno matamu na ya
kilaghai,pasipo vitendo.
AMKA TANZANIA,TUMPE KURA ZA NDIO Dr.W.SLAA,SILAHA YA UKWELI.
Nawatakieni USIKIVU,na UTEKELEZAJI mwema.

hii imekutwaq ikizungungushwa kupitia barua pepe za watu mbalimbali. Sisi tunahoji nini tatizo la watanzania na hatima ya haliyao??

HUYU RIDHIWANI KIKWETE NI NANI???

kushoto ni Yusuf masauni Mwenyekiti wa UVCCM aliyelazimishwa kujiuzuru May 2010, kulia ni Ridhiwani mtoto wa Mwenyekiti wa CCM naq Rais wa tanzania JK kikwete. Pia ni mdamini wa Mali zote za UVCCM

kulia ni Yusufu Masauni Mwenyekiti wa UVCCM aliye lazimishwa kujiuzulu, kulia ni Ridhiwani Kikwete, Mtoto wa mwenyekiti na wa CCM na Rais wa Tanzania na mlezi wa mali zote za UVCCM

Lidhiwani Kikwete ambaye ni Mjumbe wa kamati KUU ya CCM na mtoto wa mwenyekiti wa Chama hicho Rais Jakaya Kikwete amekuwa gumzo kila mara.

Sisi tunahoji huyu kijana ni nani hasa? “Ridhiwani Kikwete ni nani” Kijana huyu amekuwa akituhumiwa kuwa na kundi lililo vuruga uchaguzi ndani ya jumuiya ya UVCCM miaka michache iliyopita. Mtoto huyu ametuhumiwa pia kuwa chanzo cha vurugu ambazo zilisababisha Mwenyekiti wa UVCCM bwana Masauni aachie ngazi mapema mwaka huu.

Kana kwamba haitoshi sasa ametajwa tena kuhusika na sakata la kuenguliwa kwa mgombea ubunge Hussein Bashi kwa sababu ya kutokuwa mtanzania. Katika sakata hili pia bashi kaenguliwa kwa kuwa si Mtanzania. Ukigombana na Ridhiwani tu unakuwa mashakani. Kama unataka ufalme lamba miguu ya Ridhiwani tu hakuna noma kila kitu kinakuwa tambarare. Utakula kuku kwa mrija.

Sisi tunahoji huyu kijana ninani? Je ni ujumbe tu ndani ya UVCCM au ujumbe tu ndani ya Kamati kuu ya CCM? Kama ni hivyo ni nini basi yeye awepele abisa kusababisha hizi sintofahamu na mikwaruzo. Kama ni hivyo mbona wapo wajumbe wengi ambao hawasababishi vurugu kama hizi. Huyu ninani? CCM inafikiria juu ya vurugu hizi au kuna nini ndani yake?? Tuna mashaka sana juu ya tabia hizi na wengi tuna hiji zikiachwa nini kitafuata???

Sijui waungwana sisi kaziyetu kuhoji tu

KAMA MTI MBICHI HUFANYWA HIVI ITAKUWAJE KWA MTI MKAVU. CCM steal votes from one another how will it be to Non CCM members in General Election?

Kura za maoni na mapendekezo ndani ya ccm zimeisha nakuacha majeraha kibao sio tu kwa CCM bali kwa taifa nzima.

Tumeshuhudia rafu nyingi sana katika kipindi kuelekea uchaguzi kama ilivyo katika chaguzi zilizo pita mwaka huu tena tumepata kujua watanzania wasio watanzania  Hussein Bashi ni mfano dhairi.

CCM ina vituko visivyo na kifani. CCM inekubwa na jinamizi la kula rushwa, kwakuwa kuna makundi kundi lile lisilo nanguvu ndilo wagomdea wake wamefikishwa mahakamani au kukamatwa kwa rushwa ingawaje wote wamecheza rafu. Audha wale ambao hawakuwa na makundi huku wameshindana wa wagombea wenye makundi mambo yanakuwa magumu sana. Kashifa za uraia, ngono, ufisadi na matusi na tuhuma za kila aina zilikuwa kama vibwagizo vya kampeni zao.

Kama wao ndo wamepita kwa njia kama hizo ninini kitakacho wafanya wajiwa Bungeni waweze tetea wanyonge?

Tuhuma za kufoji  kadi za CCM tuhuma za kuiba kura na kile wanachokiita kufaurisha kura vilitamalaki mchakato mzima wa kuwapata wagombea.

Kunasehemu ambazo wanasemekanika TAKUKURU walikuwa wanadhibiti rushwa isionekane kwa watu. TAKUKURU ilikuwa inalinda watoa rushwa hasa watabaka Fulani ambao nao walipewa kitu kidogo ili maisha yaendelee. Wapi mtanzania wa kawaida atapata fursa ya kutumikiwa na kutoa maoni yake kwa uhuru na uwazi??

Taasisi ya kuzuia na kupambambana na rushwa imekuwa ikizuia watu wasione reshwa iliyotolewa. Ilidhibiti wale walio na mdomo wa kuonyesha wengine wametoa rushwa.

Kwa mantiki hii nini hatima ya nchiyetu??

Chama tawala kimefanya ufisadi huu mkubwa. Hali itakuwaje itakapofika kwa uchaguzi mkuu ambapo CCM itakuwa ina pingana na vyama vingine ambavyo tena havija pewa uwanja ulio sawa katika kushiriki uchaguzi na demokrasia nchini? Tukiwa tunajua mti mkavu ni dhaifu kuliko mbichi tunahiji Kama mti mbichi hufanywa hivi itakuwaje kwa mti mkavu?